FAQ

SWAHILI

MDAU ANASEMA:

Nimeonelea nijaribu kueleza misingi na matarajio ya Tamasha la Kimataifa la Sinema Zetu (SzIFF) ili kujibu baadhi ya maswali ya wadau. Nitatumia point kadha zilizouliziwa ili kufafanua.

 1. Je wanaonesha filamu watalipwa?

  Waonyesha filamu hawatalipwa kwa kuonyesha filamu zao kwnye shindano. Filamu hizi zinaonyeshwa kama sehemu ya mashindano. Si filamu zote zitakazoletwa zitaingia kwenye mashindano maana kuna vigezo maalum ili kufikia kiwango cha kushindanishwa kwenye tamasha. Huo ndio msingi wa Tamasha la mashindano. Tamasha linakubali filamu zilizokwisha tengenezwa tangu 2015 hadi sasa kwa sababu hatukutaka kubana nafasi ya filamu kushindanishwa. Miaka ijayo pia filamu zitakazoonyeshwa zitakuwa za miaka zaidi ya mwaka ule wa mashindano kwa sababu kuna sababu nyingi mtu anashindwa kuiwasilisha kazi yake mwaka fulani.

  Na hili sio geni katika matamasha. Ni kawaida. Vile vile ni kawaida kwa filamu kuingizwa kwenye tamasha hata kabla haijaenda kwenye hadhara. Hapo ndipo tunapotakiwa kuelewa dhana (concept) nzima ya tamasha. Tamsha linaipa filamu na tasnia kwa ujumla nafasi ya kupimwa na wengine na kupewa nafasi ya kutazamwa na wadau wa aina Fulani. Wanaokwenda Zanzibar kwa ZIFF ni wale wanaopenda kwenda Unguja kushiriki na kuona filamu zinazoonyeshwa pale. Ni aina Fulani tu za filamu na kwa kipindi Fulani tu. Vivyo hivyo na Sinema Zetu. Filamu zinazoshindanishwa zitaonyeshwa kati ya saa 1 jioni hadi saa 6 usiku- filamu hazitazidi 3 kwa siku. Ni kwa ajili ya wale ambao kwanza wana muda wa kuangalia, wenye hamu ya kujua nini tasnia ya filamu Tanzania na Afrika Mashariki inafanya, na wapenzi wa Sinema Zetu ndio watakaokwenda kuzitazama.

 2. Tamasha kwenye Televisheni- Festivals kwenye Tv ni concept mpya- haziko nyingi. (Kuna New York Tv Film Festival na nyingine chache. Hii ni ya kwanza Afrika.) Kama tamasha lolote lile kwanza unaangalia kwa nini lile tamasha limeanzishwa na malengo yake. Kwa tamasha hili nia na malengo yake ni kukuza tasnia ya filamu za Kiswahili Tanzania na Afrika Mashariki na kukuza utaifa. Filamu zinashindanishwa ili kuweka kipimo cha ubora wa filamu katika tasnia. Bila kuwa na vipimo kama hivyo tasnia itaendelea kudorora.

  Mwulize Amil Shivji kama alililipwa alipoipeleka filamu yake kwenye matamasha tofauti. Lakini mwulize pia ni faida gani alizopata kwa filamu yake kwanza kuingia kwenye tamasha, mbali na kushinda. Nia za Tamasha hili ni tofauti, na kwa hapa nia yake ni utaifa na kuinua viwango vya tasnia.

  Hata hivyo Tamasha limeonelea kuwapa hongera wote wale ambao filamu zao zitainghia duru ya pili ya mashindano- nominated films- kwa kumpa kila mwenye filamu kwenye duru hiyo Tsh100,000.

 3. Filamu mpya zinazotoka- Je pia zitaonyeshwa? Swala la filamu mpya kuonyeshwa kwa watazamaji kabla haijaonyesha kwenye hadhara limejibiwa hapo juu pia. Uwamuzi ni wa mwenye filamu. Kuionyesha filamu yako ni kwa ajili ya kuishindanisha. Haki miliki yako bado unabakia nayo na kuionyesha kwenye tamasha kamwe haipunguzii filamu yako soko. In fact inaizidishia maana inasema tayari imeingia katika mashindano kwa sababu ilifikia kiwango fulani na kukubalika. Watu wengi wanalilia kuonyesha filamu zao kwenye matamasha na in fact wanalipa kuingiza filamu zao. Kwa ZIFF wanalipa EURO5 ili filamu zao zionyeshwe kwenye tamasha. Hawalipwi zikionyeshwa. Kuna matamasha yanayolipa wenye filamu kuonyesha filamu zao kwenye tamasha lakini sio mengi na mara kwa mara ni kwa ajili ya filamu mbazo tayari mwenye tamasha anaionyesha akitarajia watu watakuja kuiona ikionyeshwa pale. Hata kwa hapo filamu inaweza kuwa kubwa sana lakini malipo yake yanaweza kuwa sawa na yeyote ile inayoonyeshwa kwenye hilo tamasha. Hatutofautishi ukubwa au wingi wa pesa iliyotengenzea filamu.

 4. Umuhimu na kazi ya matamasha- Bila kupoteza muda mrefu hapo juu nimeelezea umuhimu na kazi ya matamasha. Tamasha ni jukwaa muhimu la Tasnia kwa wadau an hasa "independent filmakers" na wenye msimamo maalum na nia ni kujenga watazamaji wapya wa filamu za aina fulani. Hapa tunajenga watazamaji wa filamu za lugha ya Kiswahili na zenye maudhui ya utaifa na utamaduni wa Mwafrika.

 5. Je filamu mpya pia zinaweza kutumwa? Ndio- Watengeneza sinema wengi wanafanya hivyo. Yaani wanazipeleka kwenye matamasha kabla ya kuuza filamu zao. Huko kwenye matamasha ndiko wanakopata soko. Na hata katika tamasha hili tunamatarajio kuwa wenye Tv stesheni na hata Azam Tv wenyewe watazitazama filamu na kununua zile ambazo zimeshinda au wanazozitaka. In fact Azam Tv wameshasema wangependa kununua filamu nyingi ya zile ambazo zitakuwa zimashinda. Kwa njia hiyo kutakuwa na kugombaniwa kwa filamu na Tv stations na kwa njia hiyo kukuza soko la filamu.

 6. Malipo na Haki miliki- Haki miliki ya filamu zinabakia na yule anayezionyesha. Tamasha haichukui haki miliki ya filamu itakayoonyeshwa. Kuonyeshwa filamu popote kule hata siku moja haiwezi kuondoa au kuchukuwa hati miliki ya kazi fulani.

LA KUKUMBUKA HAPA NI KUWA TAMASHA NI JUKWAA MAALUM LINALOSHINDANISHA FILAMU ILI KUZITAMBULISHA UBORA WAKE NA KUWEKA VIWANGO KWA WANAOTENGENEZA FILAMU HASA ZILE AMBAZO HAZIKUTENGENZEZWA NA WENYE MAKAMPUNI MAKUBWA YA FILAMU.